Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Somalia yapiga marufuku uvaaji wa barakoa kwa kuhofia usalama

Somalia Yapiga Marufuku Uvaaji Wa Barakoa Kwa Kuhofia Usalama Somalia yapiga marufuku uvaaji wa barakoa kwa kuhofia usalama

Thu, 15 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Mamlaka nchini Somalia imepiga marufuku uvaaji wa barakoa katika mji mkuu, Mogadishu, kutokana na hofu ya kiusalama.

Msemaji wa utawala wa Mogadishu, Salah Dheere, alisema kuwa uvaaji wa barakoa ulikuwa unatumika kuficha utambulisho na kurahisisha vitendo vya uhalifu.

Barakoa hizo zilitumika sana wakati wa janga la Covid-19.

Mamlaka pia iliharamisha uvaaji wa kofia na kubeba silaha katika usafiri wa umma.

Hata hivyo, kofia za jadi za sunna zinazovaliwa na wazee haziruhusiwi kupigwa marufuku.

Uamuzi huo ulitolewa wakati wa mkutano wa hivi majuzi wa usalama mjini Mogadishu, ulioongozwa na Rais Hassan Sheikh Mohamud.

Somalia imekuwa ikikabiliwa na ukosefu wa usalama kwa miaka mingi, huku vitisho vikuu vikitoka kwa kundi la wanamgambo wa al-Shabab.

Kundi hilo lenye mafungamano na al-Qaeda limeongeza mashambulizi katika hali ya kuonyesha kuibuka upya tangu serikali ya Rais Mohamud ilipoanzisha mashambulizi dhidi ya kundi hilo mwezi Agosti 2022.

Chanzo: Bbc