Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Somalia yapiga marufuku meli za uvuvi za kimataifa katika pwani yake

Somalia Hnhjnjhnm Somalia yapiga marufuku meli za uvuvi za kimataifa katika pwani yake

Fri, 12 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Somalia imepiga marufuku meli za uvuvi za kimataifa katika eneo lake la bahari, ikiwa ni sehemu ya juhudi mpya za kukomesha uvuvi kupita kiasi wa samaki katika eneo hilo la Bahari ya Hindi.

Wizara ya Uvuvi na Uchumi wa Bluu Somalia imesema katika taarifa kwamba meli hazitaruhusiwa tena kuvua samaki bila idhini kutokana na uharibifu mkubwa unaosababishwa wakati wa uvuvi.

Wizara ilisema ukiukwaji wowote wa kanuni hii unaweza kukabiliwa na faini, kifungo, kutaifishwa kwa bidhaa za samaki zilizopatikana, na kunyang'anywa vifaa vya uvuvi.

Somalia ina ukanda mrefu zaidi wa pwani barani Afrika na mara nyingi samaki wake wamekuwa wakivuliwa kinyume cha sheria, kutokana kuporomoka mfumo wa usalama nchini humo baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kuanza 1991.

Somalia ina wasiwasi kuwa kuvua samaki kupita kiasi kuharibifu wa mazingira ya baharini na kupunguza idadi ya samaki. Aidha uchunguzi umebaini kuwa baadhi ya nchi tajiri pia zilikuwa zikitupa taka katika pwani ya Somalia. Hata hivyo kutakuwa na changamoto katika kutekeleza marufuku hiyo kwa sababu eneo lililojitenga Somaliland ambalo limejitangazia uhuru na mamlaka inayojiendesha ya Puntland hutoa leseni za uvuvi kwa mashirika ya kimataifa bila kuitarifu serikali kuu iliyoko Mogadishu.

Serikali ya Somalia pia ina wasiwasi kwamba vikosi vya wanamaji vya NATO vinavyoongozwa na Marekani vinavyodai kupambana na uharamia vimechukua hatua ndogo katika kusimamisha meli za uvuvi haramu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live