Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Somalia yajipigia chapuo kujiunga EAC

Somaliskakvinnor Fotograffeisalomarreuters 1140x640 Somalia yajipigia chapuo kujiunga EAC

Mon, 30 Jan 2023 Chanzo: Dar24

Kuchaguliwa kwa Rais Hassan Sheikh Mohamud kunaweza kushawishi utawala wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC), kuipa fursa nchi ya Somalia kujiunga na jumuiya ya umoja huo, pamoja na kuwa taasisi zake bado zinaendelea kuimarishwa.

Jumuiya ya Afrika Mashariki, tayari imeanza kutathmini ustahiki wake wa kujiunga na umoja huo kutokana na hatua hiyo ambayo inafuatia historia ya kukubaliwa kujiunga kwa Sudan kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, zote mbili zikikabiliwa na mzigo mkubwa wa kukabiliana na vita.

Ukomo magonjwa yasiyopewa kipaumbele ni 2030REA yaungana na Wadau usimamizi miradi ya UmemeNchi ya Sudan Kusini, ilikubaliwa rasmi kujiunga mwaka 2016 lakini imeshindwa kufuata kikamilifu itifaki za jumuiya hiyo.

Kwa mara ya kwanza, Somalia iliomba kujiunga na EAC mwaka 2012 lakini ilikataliwa kutokana na misukosuko inayotokana na Al-Shabaab na ukosefu wa sheria thabiti kwa wakati huo.

Chanzo: Dar24