Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Somalia yagundua na kuvunja mitandao ya Al-Shabab

Somalia Yagundua Na Kuvunja Mitandao Ya Al Shabab Somalia yagundua na kuvunja mitandao ya Al-Shabab

Fri, 2 Feb 2024 Chanzo: Voa

Idara ya kitaifa ya Ujasusi na Usalama ya Somalia, NISA, imesema AlhamIsi kwamba kwa mara ya kwanza imeweza kufunga kabisa mitandao mipya 14 inayosemekana kutumiwa na kundi la kigaidi la al Shabab.

Kupitia taarifa kwenye X, iliyojulikana kama Twitter, NISA imesema kwamba kufuatia operesheni ya usalama wa kimitandao, kitengo chake maalum cha masuala ya mitandao kimegundua mitandao inayoendesha shughuli za al Shabab, ambalo ni tawi la al Qaida, Afrika Mashariki.

Idara hiyo imeongeza kwamba operesheni yake ilihusisha uchunguzi dhidi ya mitandao yenye mashaka, pamoja na kuthibitisha wamiliki wake. Naibu waziri wa Habari wa Somalia Abdirahman Yusuf Adala ameambia VOA kwamba operesheni hiyo ni sehemu ya vita vya serikali dhidi ya ugaidi na misimamo mikali.

Hapo Jumanne, NISA ilisema pia kwamba ilifunga makundi 20 ya WhatsApp yanayosemekana kuendeshwa na al Shabab kwa madhumuni ya kupora watu, pamoja na kukandamiza. Kupitia taarifa fupi, idara hiyo iliongeza kuwa ilikatiza huduma kwenye zaidi ya simu 2,500 zinazohusishwa na kundi hilo.

Operesheni hiyo imefanyika wakati Somalia ikijitahidi kuvunja mifumo ya mawasiliano ya kundi hilo, pamoja na mitandao ya kifedha, kama sehemu ya ahadi yake ya vita kamili dhidi ya kundi hilo. Al Shabab kwa miaka mingi limeshika udhibiti wa baadhi ya sehemu za Somalia, wakati likifanya mashambulizi mabaya ya kigaidi mjini Mogadishu.

Chanzo: Voa