Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Somalia wajiunga rasmi EAC

DE1C50B9 1356 4FEF 93E6 D5E57A54CEC8.jpeg Somalia wajiunga rasmi EAC

Sat, 16 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Somalia imejiunga rasmi na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wiki tatu baada ya nchi wanachama kukubali kuingia katika Jumuiya hiyo ya kikanda

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud ametia saini mkataba wa kuipatia nchi hiyo uanachama kamili wa umoja huo Desemba 15.2023 katika hafla iliyoongozwa na mwenyekiti wa sasa wa EAC Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, nchini Uganda

Nchi hiyo ilikubaliwa kuingia EAC tarehe 24 Novemba, na kuwa mwanachama wa nane wa Jumuiya hiyo baada ya Burundi, DR Congo, Kenya, Sudan Kusini, Tanzania, Rwanda na Uganda

Rais Mohamud amesema kuwa kurasimishwa kwa ushirikiano wa Somalia katika umoja huo ni "mwanga wa matumaini kwa mustakabali uliojaa matumaini" na kwamba nchi yake inatazamia kuchangia maendeleo ya eneo hilo

Chanzo: www.tanzaniaweb.live