Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Somalia ni waathirika wa mabadiliko ya hali ya hewa - UN

Somalia Ni Waathirika Wa Mabadiliko Ya Hali Ya Hewa   UN Somalia ni waathirika wa mabadiliko ya hali ya hewa - UN

Tue, 11 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema watu wa Somalia ndio wahanga wakubwa wa mabadiliko ya tabianchi licha ya kutochangia mabadiliko hayo.

Ujumbe wa Nukuu: Ingawa Somalia haitoi mchango wowote katika mabadiliko ya hali ya hewa, Wasomali ni miongoni mwa waathirika wakubwa"

Bw Guterres alitoa wito wa kuungwa mkono kwa wingi kimataifa mwanzoni mwa Ziara ya nchi hiyo katika hali ya ukame mkubwa.

Umoja wa Mataifa umezindua ombi la mabilioni ya dola kwa Somalia ambako mamilioni wanakabiliwa na njaa.

Ujumbe wa Nukuu: Takriban watu milioni tano wanakabiliwa na viwango vya juu vya uhaba wa chakula, na bila shaka kupanda kwa bei kunafanya mambo kuwa mabaya zaidi.

Takriban watu milioni tano wanakabiliwa na viwango vya juu vya uhaba wa chakula, na bila shaka kupanda kwa bei za bidhaa kunafanya mambo kuwa mabaya zaidi.

Ujumbe wa Nukuu: Kwa hivyo, natoa wito kwa wafadhili, na ninatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuongeza uungaji mkono wao ili kufadhili haraka mpango wa kukabiliana na misaada ya kibinadamu wa 2023, ambao kwa sasa unafadhiliwa kwa asilimia 15 tu."

Kwa hivyo, ninatoa wito kwa wafadhili, na nitoe wito kwa jumuiya ya kimataifa kuongeza uungwaji mkono wao kufadhili haraka mpango wa kukabiliana na misaada ya kibinadamu wa 2023, ambao kwa sasa unafadhiliwa kwa asilimia 15 tu."

. Somali National TVCopyright: Somali National TV Awali, Antonio Guterres aliandika kwenye akaunti yake ya Twitter kwamba ziara yake nchini Somalia inaendana na desturi yake ya kila mwaka ya kutembelea nchi za Kiislamu wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa "kufunga kwa mshikamano na kushiriki Iftari."

Wizara ya Mambo ya Nje ya Somalia ilisema umuhimu wa ziara hiyo ni 'kufanya mazungumzo ya kisiasa, usalama, maendeleo na kibinadamu'.

Bwana Guterres amekutana na Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud.

Kuhusu uasi wa Kiislamu, serikali ya Somalia imepata mafanikio katika vita vyake na Al-Shabaab, hasa katikati mwa Somalia.

Kulingana na Crisis Group, maendeleo mengi yametokana na kutoridhika kwa wenyeji na kundi hilo, ambako kumesababisha kuundwa kwa wanamgambo wa koo ambao tangu wakati huo wameunda muungano kurudisha nyuma Al-Shabab.

Chanzo: Bbc