Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Somalia kutaka kumaliza Al-Shabab, Desemba mwakani

Somalia Kutaka Kumaliza Al Shabab, Desemba Mwakani Somalia kutaka kumaliza Al-Shabab, Desemba mwakani

Wed, 22 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Somalia ina mwaka mmoja kuweza kumaliza uwasi unaofanywa na kundi la wanamgambo wa al-Shabaab wenye uhusiano na al-Qaeda kutoka nchini humo, rais Hassan Sheikh Mohamud amesema Jumanne.

Hayo yakiendelea muda wa mwisho wa wanajeshi waliosalia wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika kuondoka ukikaribia Desemba.

Rais Mohamud, akiwa anahudumu muhula wake wa pili, amesema mwezi Agosti alitaka kukimaliza kundi hilo mapema mwaka ujao.

Muda wa mwisho ni Desemba 2024 wakati kikosi cha ATMIS kinapaswa kuondoka nchini humo, rais Mohamud aliwambia wajumbe kwenye mkutano ulofanyika katika taasisi ya Royal United Services ya London.

Lengo lilikuwa kumaliza wapiganaji walobaki wa al Shabaab, aliongeza kusema.

Kazi hiyo ilifanywa kuwa ngumu zaidi na mafuriko mabaya ya hivi karibuni, ingawa pia yamefanya kuwa vigumu kwa wanamgambo hao kuendeleza mashambulizi ya mabomu ya ardhini, alisema.

Chanzo: Bbc