Chini ya mkataba huo wa miaka kumi, Uturuki itavipa silaha na kutoa mafunzo kwa vikosi vya jeshi la wanamaji la Somalia na kupeleka meli zake katika maji ya Somalia.
Wachambuzi wanasema ni hatua kubwa katika kuimarisha usalama wa baharini wa Somalia.
Waziri Mkuu Hamza Abdi alisema mpango huo unaondoa - kwa maneno yake - hofu ya ugaidi, uharamia, uvuvi haramu na utupaji wa taka za sumu.
Inakuja wakati Ethiopia ilitia saini makubaliano yenye utata na jamhuri iliyojitangaza ya Somaliland, ambayo imeongeza mvutano kati ya Mogadishu na Addis Ababa. (Somalia, ambayo inaichukulia Somaliland kuwa sehemu ya eneo lake, imeishutumu Ethiopia kwa kukiuka mamlaka yake).