Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Somalia:Tunajaribu kukomesha machafuko Somaliland

Rais Somaliaaa Somalia:Tunajaribu kukomesha machafuko Somaliland

Wed, 8 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia amesema kuwa nchi hiyo inajaribu kurejesha amani katika eneo lililojitenga na nchi hiyo la Somaliland kaskazini mwa nchi kufuatia kuibuka mivutano kati ya mamlaka za utawala na makundi ya koo katika eneo hilo.

Rais Hassan Sheikh Mohamud amesema, umoja ndio njia pekee itakayopelekea kupatiwa ufumbuzi hali ya sasa huko Somaliland.

Machafuko yaliibuka mwezi uliopita katika eneo la Somaliland baada ya viongozi wa majimbo ya Sool, Sanaag na Cayn katika eneo hilo lililojitenga na Somalia mwaka 1991, kutangaza nia yao ya kutaka kujiunga tena na Somalia.

Mapigano ya mwezi uliopita katika mji wa Lascanood katika jimbo la Sool yaliua watu wasiopungua 80 na kupelekea zaidi ya 185,000 kuhama makazi yao. Imeelezwa kuwa hali ya mvutano imejitokeza katika miezi ya hivi karibuni, na kusababisha mapigano kati ya vikosi vya jeshi la Somaliland na vikundi vinavyoitii serikali ya Somalia, haswa katika eneo la Las Anod.

Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia ameongeza kuwa kwa wiki kadhaa sasa kunafanyika juhudi za kukomesha mapigano na kutoa mwanya wa kufanyika mazungumzo huko Somaliland. Rais wa Somalia pia ameashiria mapambano ya serikali yake dhidi ya kundi la al-Shabaab, ukame mkubwa ulioiathiri Somalia na unyanyasaji wa kijinsia nchini humo.

Agosti mwaka jana, miezi kadhaa baada ya Rais Mohamud wa Somalia kuchaguliwa kwa mara ya pili, alitangaza vita vya pande zote dhidi ya wanamgambo wa al Shabaab ambao wamekuwa wakifanya hujuma na mashambulizi mara kwa mara dhidi ya serikali tangu mwaka 2007.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live