Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Somalia, Sudan zalaani mauaji ya kiongozi Mkuu Hamas

Hamas Teharan.jpeg Somalia, Sudan zalaani mauaji ya kiongozi Mkuu Hamas

Thu, 1 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nchi mbili za Somalia na Sudan zimeungana na nchi nyingine nyingi duniani kulaani kwa maneno makali jinai ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kumuua kidhulma na kigaidi Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS aliyekuwa ziarani hapa Tehran.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Somalia imetuma mkono wa pole kwa taifa la Palestina na kulaani vikali jinai hiyo ya Israel ikisisitiza kuwa, mauaji hayo ya kigaidi yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni ni uvunjaji wa wazi wa sheria zote za kimataifa.

Sehemu moja ya taarifa hiyo imesema kuwa, Mogadishu inalaani mauaji na vitendo vyote vya machafuko kwa sura zake zote na kwa kisingizio chochote kile.

Vilevile imetilia mkazo wajibu wa jamii ya kimataifa kutekeleza ipasavyao majukumu yake na kuchukua hatua za haraka za kukomesha jinai za israel huko Ghaza na uvunjaji wake wa wazi wa sheria za kimataifa.

Kwa upande wake, Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan jana ilitoa taarifa rasmi na kulaani vikali mauaji ya kigaidi yaliyofanywa na Israel dhidi ya Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya HAMAS, Ismail Haniyeh, hapa Tehran.

Sehemu moja ya taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan imesema: "Serikali ya Sudan inalaani jinai ya mauaji ya Kiongozi wa Kisiasa wa HAMAS mjini Tehran."

Taarifa hiyo imesisitiza pia kwamba Khartoum inapinga na kukemea kitendo chochote cha kuua wapinzani wa kisiasa kwa kisingizio chochote kile.

Ismail Haniyeh, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS alikuwepo hapa Tehran kuhudhuria sherehe za kuapishwa Rais wa 14 wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Masoud Pezeshkian.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live