Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Somalia: Atmis imekabidhi kambi tisa kwa jeshi la serikali

Au Au Somalia Kusepa.jpeg Somalia: Atmis imekabidhi kambi tisa kwa jeshi la serikali

Wed, 31 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ujumbe wa Umoja wa Afrika nchini Somalia (Atmis) umesema umekabidhi kambi tisa za kijeshi kwa serikali ya Somalia, kuashiria kukamilika kwa awamu ya pili ya kuondoka kwa wanajeshi wake nchini humo.

Kambi saba kati ya tisa zilikabidhiwa Jumatatu ya wiki hii katika hafla iliyofanyika Mogadishu, mji mkuu wa Somalia, Atmis ilisema katika taarifa yake.

Miongoni mwa maeneo yaliyokabidhiwa kwa vikosi vya usalama vya Somalia ni pamoja na Ikulu, ofisi za bunge, uwanja wa ndege wa Kismayo, Bia Cadale na Burahache.

Kulingana na Atmis, vituo vingine viwili vya kijeshi vilivyofungwa ni Sarille na Old Airport iliyokuwa chini ya vikosi vya KDF.

Alhaji Sarjoh Bah, mkurugenzi wa usimamizi wa migogoro ndani ya Idara ya Masuala ya Kisiasa, Amani na Usalama ya Tume ya Umoja wa Afrika, alisema uondoaji huo unaashiria hatua muhimu katika mwelekeo mzuri wa Somalia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live