Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Somalia, AU na UN kuanza awamu ya pili ya kupunguza wanajeshi

Au Au Somalia Kusepa.jpeg Somalia, AU na UN kuanza awamu ya pili ya kupunguza wanajeshi

Mon, 4 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Somalia, Kikosi cha Mpito cha Umoja wa Afrika (ATMIS), na Ofisi ya Misaada ya Umoja wa Mataifa (UNSOS) jana Jumamosi kwa pamoja zilitangaza kuanza awamu ya pili ya kuondoka wanajeshi wa kigeni nchini humo mwezi huu wa Disemba.

Mohammed El-Amine Souef, mwakilishi maalumu wa Mwenyekiti wa Kamisheni ya AU huko Somalia ambaye pia ni mkuu wa ATMIS amesema kwamba, mchakato wa kuwaondoa wanajeshi wengine 3,000 kutoka Somalia awali ulikusudiwa kukamilika mwishoni mwa Septemba lakini ulisitishwa kufuatia ombi la serikali ya Somalia kwa sababu za kiufundi.

Souef alisema hayo jana mjini Mogadishu na kuongeza kuwa, baada ya majadiliano ya kina ya kiufundi baina ya pande tatu hizo, na kwa kuzingatia maagizo ya Umoja wa Afrika na Azimio nambari 2710 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la mwaka (2023), leo tunatangaza kwa pamoja kuwa ATMIS itaanza tena mchakato wa kukamilisha zoezi la kuondoka askari 3,000 nchini Somalia, ifikapo Desemba 31, 2023.

Kwa mujibu wa taarifa ya pamoja iliyotolewa baada ya mkutano huo, Souef amesema kuwa tangu kusitishwa kiufundi mchakato huo mwezi Septemba, ATMIS, serikali ya Somalia na UNSOS wameshirikiana kwa karibu kuweka hatua za kurejesha mchakato wa kuvikabidhi majukumu vyombo vya serikali ya Somalia kama ilivyoelezwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na AU.

Katika awamu ya kwanza ya zoezi hilo ambalo lilikamilika mwezi Juni, ATMIS iliondoa wanajeshi 2,000 na kukabidhi udhibiti wa kambi saba za kijeshi kwa Vikosi vya Usalama vya Somalia, kama ilivyoamriwa na maazimio 2687 na 2670 ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live