Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Solskjaer amkingia kifua De Gea

97633 Pic+degea Solskjaer amkingia kifua De Gea

Mon, 2 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

London, England. Licha ya kufanya kosa, Ole Gunnar Solskjaer amesema David De Gea ndiye kipa namba duniani.

De Gea alifanya kosa lililogharimu baada ya kupiga mpira vibaya  ambao ulinaswa na mchezaji wa Everton na kuruhusu bao la kwanza.

Pamoja na kufanya kosa hilo, kocha huyo alisema De Gea ndiye kipa bora kwake. Manchester United na Everton zilitoka sare ya bao 1-1.

Solskjaer alisisitiza kuwa licha ya kufanya makosa kwake ni kipa bora mwenye kiwango cha kushindana duniani.

Nahodha wa zamani wa Man United, Roy Keane alisema De Gea hana thamani katika eneo hilo kutokana na kosa hilo.

De Gea alifanya kosa kwa kupiga vibaya aliorudishiwa na  Harry Maguire na kutoa nafasi kwa Dominic Calvert-Lewin kufunga bao ikiwa ni dakika ya tatu kabla ya Bruno Fernandes kusawazisha.

Pia Soma

Advertisement

Hata hivyo, kipa huyo wa kimataifa wa Hispania aliomba radhi kwa mashabiki muda mfupi baada ya kosa hilo.

“Msimu uliopita alikuwa katika presha kubwa, lakini ukiniuliza msimu huu amefanya kosa gani sikumbuki. Namuamini David kwa asilimia 100,”alisema Solskjaer.

Chanzo: mwananchi.co.tz