Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Siwezi! na siwezi! Rais Uhuru akaa ngumu kuhusu kuidhinisha majaji 6 waliosalia

D637ce347a0bc263 Siwezi! na siwezi! Rais Uhuru akaa ngumu kuhusu kuidhinisha majaji 6 waliosalia

Tue, 15 Jun 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Uhuru alisema dhamira yake haiwezi kumruhusu kuwaidhinisha majaji sita waliosalia baada ya kupokea ripoti kadhaa kutoka kwa idara za usalama dhidi yao Uhuru alikatakaa kuwateua majaji George Odunga, Joel Ngugi, Aggrey Muchelule, Weldon Korir, Makori Evans Kiago, na Judith Omange Cheruiyot Msimamo wa Uhuru unakujia wakati analimbikiziwa presha na wakosoaji wake ikiwemo Jaji Mkuu Martha Koome

Rais Uhuru Kenyatta amesisitiza kuwa hatawaidhinisha majaji sita ambao walipendekezwa kupandishwa cheo kuwa majaji wa Mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu.

Mnamo Juni 3, kiongozi wa taifa alikataa uteuzi wa George Odunga, Joel Ngugi, Aggrey Muchelule, Weldon Korir, Makori Evans Kiago, na Judith Omange Cheruiyot kwa msingi wa kimaadili.

Akizungumza wakati wa mkutano na viongozi wa Ukambani katika Ikulu ya Nairobi, Jumatatu, Juni 14, Uhuru alisema dhamira yake haiwezi kumruhusu kuwaidhinisha majaji sita waliosalia baada ya kupokea ripoti kadhaa kutoka kwa idara za usalama dhidi yao.

Msimamo wa Uhuru unakujia wakati analimbikiziwa presha na wakosoaji wake wakidai kukataliwa kwa majaji hao ni kinyume cha katiba.

Wale ambao wanashinikiza kuidhinishwa kwa sita hao ni ikiwemo Jaji Mkuu Martha Koome watangulizi wake David Maraga and Willy Mutunga miongoni mwa wanasheria wengine.

Katika taarifa siku ya Ijumaa, Juni 4, Koome alitaja mrundiko wa kesi kutokana na uhaba wa majaji akidai kutoteuliwa kwa sita hao kutaathiri Idara ya Mahakama.

"Mimi ni jaji na sitaki kuingia kwenye mabishano yoyote lakini nina jukumu la kusisitiza msimamo wangu wa kumtaka (Rais) Uhuru awateue majaji sita waliosalia," alisema.

Fauka ya hayo, Koome alisema kuna haja ya kutafuta suluhu ya kudumu ili kuzuia kucheleweshwa kwa uteuzi wa majaji siku za usoni.

Jaji Mkuu wa zamani Willy Mutunga alikuwa amependekeza Uhuru ang'olewe mamlakani kwa kukiuka sheria.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke