Afrika Kuisni imesisitiza juu ya udharura wa kushughulikiwa kisheria jinai za Utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi wasiokuwa na hatia wa Palestina katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC yenye makao makuu yake huko The Hague nchini Uholanzi.
Kushtadi jinai za hivi sasa za utawala katili wa Isreal dhidi ya wananchi wa Palestina hasa katika Ukanda wa Gaza kumeibuia ghadhabu na hasira za waliowengi ulimwenguni.
Wizara ya Sheria ya Afrika Kusini ilitangaza Jumatano usiku kwamba jinai za Israel lazima zichunguzwe na kushughulikiwa bila ya ubaguzi wala upendeleo wowote na Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai.
Wizara hiyo imezitaja jinai za kutisha na kinyama za Israeli huko Gaza kuwa ni jinai za kivita kwa mujibu wa sheria za jinai za kimataifa. Jinai za Israel dhidi ya watoto wa Palestina
Wizara ya Sheria ya Afrika Kusini pia imeelezea wasiwasi wake kuhusiana na utendajikazi wa Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai katika kukabiliana na suala la Palestina.
Idara ya habari ya serikali ya Palestina huko Gaza imetangaza karibuni kuwa jeshi la Israel limehusika na jinai za kivita 77 na mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina tangu kumalizika usitishaji vita wa muda huko Gaza ambapo matokeo yake yamekuwa ni kuuawa shahidi watu 1,240.
Kwa msingi huo idadi ya mashahidi wa Palestina tokea kuanza operesheni ya Kimbunga cha Al Aqsa tarehe 7 Oktoba hadi sasa imefikia watu elfu 16 na 248.