Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sisi ashinda muhula wa tatu kama rais wa Misri

Sisi Ashinda Muhula Wa Tatu Kama Rais Wa Misri Sisi ashinda muhula wa tatu kama rais wa Misri

Mon, 18 Dec 2023 Chanzo: Bbc

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi ameshinda muhula wa tatu, na kupata chini ya asilimia 90 ya kura, katika uchaguzi uliofanyika wiki iliyopita, tume ya uchaguzi imetangaza.

Kulikuwa na wagombea watatu waliokuwa wakigombea dhidi yake - lakini hakuna hata mmoja wao aliyechukuliwa kuwa mtu mkuu.

Bw Sisi alikua rais kwa mara ya kwanza mwaka 2014 - ambapo alishinda kwa 97% ya kura. Alishinda kwa kiwango hicho hicho mwaka wa 2018.

Ushindi huu unamaanisha kuwa atakuwa mamlakani hadi 2029, atakapozuiwa na katiba kugombea tena.

Chanzo: Bbc