Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simulizi za DP Ruto zilizowaacha wageni kwa kicheko wakati wa harusi ya bintiye

69e4d5e6d245bc7b Simulizi za DP Ruto zilizowaacha wageni kwa kicheko wakati wa harusi ya bintiye

Sat, 29 May 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Ruto alisema kisa cha Chinedu kilimfanya kuhofia dume kutoka Nigeria na haikuwa rahisi kupeana June kwa Alex

- Aliwaacha wageni wakivunja mbavu baada ya kuwasimulia kisa cha Chinedu na alivyohisi kuhusu watu kutoka Igbo

- DP alimtaka bintiye kuwa mke mwenye heshima na mnyenyekevu pale nyumbani

Naibu Rais William Ruto ni mmoja wa wanasiasa nchini ambao wana ulimi unaoweza kuwavunja mbavu wanaomskiza.

Ni chombo ambacho amekuwa akitumia kuwayeyusha roho wengi na hata kujipatia ufuasi wa kisiasa.

Hali ilikuwa kama hiyo Alhamisi Mei 27 katika jumba la Hustler's Mansion kule mtaani Karen wakati wa kumpoza bintiye June Ruto.

Alisimulia kuwa haikuwa rahisi kwake kumpeana bintiye kwa kwa dume na hata ngumu zaidi baada ya kugundua ni kutoka Nigeria.



Alisema awali alihofia kupeana June kwa Alex Ezanagu kwa sababu ya kile serikali ilipitia na mfanyibiashara Antony Chinedu.

"Niko katika hali ya furaha na hofu kiasi. Si rahisi kwa mzazi kupeana msichana wako. Na ni ngumu zaidi iwapo unampeana kwa dume kutoka Nigeria," alisema DP na kuwaacha wageni kwa kicheko.

"Na sasa ni ngumu zaidi iwapo dume huyo ni kutoka eneo la Igbo," aliongeza DP.

Viongozi wa Nyanza



Aliwaelezea wageni ni kwa nini alikuwa na hofu moyoni kuhusu dume kutoka Nigeria na haswa kutoka eneo hilo la Igbo

"Mara ya kwanza kukutana na Alex nilimwambia kuhusu jamaa aliyekuwa akiitwa Chinedu ambaye alitusumbua sana na nilikuwa nimearifiwa ni kutoka Igbo.

"Sasa mnaweza kunielewa . . . huyu Chinedu alitupa shida sana na tulipomsafirisha kwao Nigeria alikataa hadi kushuka ndege pale Lagos kwa siku mbili. Baada ya kumwacha huko, tena tulimpata hapa Kenya," alisema huku wageni wakiendelea kuvunja mbavu.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama habari kemkem za TUKO hapa

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke