Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simulizi ya watu wanaoishi na simanzi Sudan Kusini kwa miaka 10

Huzuni Sudan Simulizi ya watu wanaoishi na simanzi Sudan Kusini kwa miaka 10

Thu, 30 Dec 2021 Chanzo: BBC Swahili

Juni 2011, taifa hilo la watu milioni 11 lilitangaza uhuru wake kutoka kwa Sudan, kufuatia kura ya maoni ambapo karibu 99% ya wapiga kura walichagua kujitenga.

Tangu wakati huo, ameishi kupitia majanga baada ya majanga juu ya majanga.

Muda mfupi baada ya kutangaziwa uhuru huo, vita vya wenyewe kwa wenyewe vilizuka ambavyo vimesababisha vifo vya mamia kwa maelfu huku mamilioni ya watu wakiwa na majeraha mioyoni na ya kimwili na baadhi kukimbia makazi yao.

Emmanuel ni mmoja wa watu wengi wa Sudan Kusini ambao wamathirika na na mzozo huo uliomalizika kinadharia kwa kusainiwa tu ili kusitishaji mapigano mwaka 2018, lakini ukweli bado unaendelea kutesa maisha yake.

Katika mahojiano na BBC, Emmanuel mwenye umri wa miaka 37 anasimulia "vitendo vya kikatili" vingi ambavyo amepitia na kulazimika kuondoka nyumbani kwake baada ya kupokea vitisho kutoka kwa kundi lenye silaha katika jimbo la Magharibi ya Equatoria, kusini. -magharibi mwa nchi.

Anasema aliona watu wakiuawa na "kukatwa vipande vipande."

"Wajawazito waliokuwa wanachinjwa walikatwa katwa na kisha kuwachinja watoto wao ambao walikuwa bado tumboni," anasema.

"Kulikuwa na watoto ambao waliuawa mbele ya mama zao na watu ambao walipigwa mabomu ndani ya nyumba zao."

"Yote haya yameniletea majeraha yasiyofutika," anaongeza. "Lakini kwa kuwa mimi ni mtaalamu wa tiba, nimeweza kuachana na hilo kwa sababu nimesoma vitabu vingi vya uponyaji wa majeraha.

Miaka kumi baada ya kuundwa kwake, Sudan Kusini ndiyo nchi changa zaidi duniani na moja ya nchi maskini zaidi na zisizo imara, licha ya kuwa na akiba kubwa ya mafuta.

Kutoka kwa mzozo wa kisiasa hadi mzozo wa kikabila

Baada ya kutangaza uhuru wa Khartoum, kundi la waasi wa zamani, ambao walikuwa kama viongozi katika eneo hilo, walijiunga na mipango ya serikali mpya ya kujenga taifa jipya na lenye ustawi zaidi.

Sudan Kusini ni taifa lenye utajiri wa mafuta na wasiwasi wa awali wa serikali ya nchi hiyo changa ulikuwa kudumisha uzalishaji.

Lakini kwa hili ilibidi kusuluhisha msururu wa kutoelewana na Sudan, Baada ya kuwa huru, Sudan Kusini ilichukua zaidi ya 75% ya hifadhi yote ya mafuta.

Wasudan Kusini, hata hivyo, walihitaji vifaa vya mafuta na bandari ya Khartoum ili kusafirisha madini .

Mbali na mzozo huu, pia kulikuwa na uasi wa kutumia silaha, mapigano ya mipakani, na kugombania udhibiti wa mifugo.

Hali ilizidi kuwa mbaya baada ya kutoelewana katika chama tawala cha SPLM kilichopelekea Rais Salva Kiir wa kabila la Dinka (kundi kubwa kuliko yote nchini) kumuondoa Makamu wa Rais Riek Machar, mwanachama wa kabila la pili kwa ukubwa la Nuer, Julai 2013.

Kiir alimshutumu makamu wake wa rais kwa kupanga mapinduzi na kile kilichoanza kama mzozo wa kisiasa kiligeuka haraka kuwa mzozo wa kikabila.

Amani ya undugu

Emmanuel, ambaye sasa anaishi katika kambi ya wakimbizi ya Umoja wa Mataifa katika mji wa Tambura, anasema kuwa baada ya kusitishwa kwa mapigano kuna "amani ya kindugu".

"Mjini mambo ni shwari, watu wanaweza kwenda sokoni na hakuna mapigano tena, lakini bado kuna hofu," anafafanua.

Kwa hakika, watu bado hawawezi kurejea majumbani mwao, nyumba nyingi zilichomwa na bado kuna makundi yenye silaha msituni.

Raia hao wa Sudan Kusini wanasema mwanzoni mwa mwezi Disemba waliwaua baadhi ya watu waliokwenda shambani na kumpiga risasi mwingine mkononi.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, licha ya kuwa takriban Wasudan Kusini milioni 2 ambao wamekimbia makazi yao ndani ya nchi kutokana na mzozo huo, idadi ya wakimbizi wa Sudan Kusini walio nje ya nchi, hasa Ethiopia, Sudan na Uganda, imepita milioni 2.2.

Wakimbizi wengi ni wanawake na watoto, na wengi wao wamevuka mpaka peke yao.

Jok Madut, profesa wa masuala ya binadamu anthropolojia katika Chuo Kikuu cha Syracuse, New York, na mchambuzi, mtaalam wa Sudan Kusini, anaelezea kwamba makubaliano ya amani ambayo yalitiwa saini mwaka 2018 yaliainisha safu ya mabadiliko ya awali katika kipindi cha mpito ambayo "hayajawahi kufanywa".

"Mipango ya usalama haijatekelezwa ipasavyo. Lakini, kilichoruhusu ghasia kuendelea ni kwamba kuna baadhi ya makundi ambayo hayakutia saini makubaliano ya amani," alisema

Makundi haya ni pamoja na National Salvation Front (NAS), ambalo limekuwa likipigana na serikali tangu 2017 na wanamgambo waliojitenga na chama cha SPLM-IO. "Walisema watatukata kama boga"

Ripoti iliyochapishwa na shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International mapema mwezi Disemba inazungumzia wimbi la hivi karibuni la ghasia kusini-magharibi mwa nchi.

Kwa mujibu wa shirika hilo, kati ya Juni na Oktoba mwaka huu pekee, makumi ya raia waliuawa na wengine wapatao 80,000 walilazimika kuyahama makazi yao kutokana na mapigano kati ya makundi yenye silaha Magharibi mwa Equatoria.

Amnesty International iliwahoji watu kadhaa walionusurika katika ripoti hiyo.

Mwanamke mwenye umri wa miaka 41 aliwaambia jinsi yeye na dadake mkubwa walivyokamatwa msituni mwezi Septemba walipokuwa wakijaribu kutoroka kutoka Tambura.

"Walituamuru tuketi na kusema watatukata kama boga."

Mwanamke huyo wa Sudan Kusini alidai kuwa watu hao waliokuwa na silaha walimfunga mikono nyuma ya mgongo wake na kumweka mtoto wake wa kiume wa miezi 18 karibu naye.

Baadaye mmoja wa wapiganaji "aliweka mguu wake juu ya kichwa (cha dada yangu) na kukata shingo yake kwa kisu."

"Ni kidogo sana cha kusherehekea"

Kana kwamba vita havikutosha, hali ya kibinadamu kwa Wasudan Kusini ilizidi kuwa mbaya mwaka 2019 kufuatia mafuriko ambayo yaliwaacha mamia ya maelfu ya watu bila makazi.

Mafuriko yameendelea kwa mwaka wa tatu mfululizo.

2021, mvua ilinyesha kwa zaidi ya miezi sita na iliathiri zaidi majimbo manne kaskazini na mashariki mwa nchi.

Kulingana na Umoja wa Mataifa, takriban watu 700,000 wamelazimika kuyahama makazi yao kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

"Kwa hiyo, unaweza kusema kwamba miaka 10 baada ya uhuru, uhuru wetu wa kisiasa unaweza kuwa sababu ya kusherehekea," anasema Profesa Jok Madut.

"Lakini tukiangazia ustawi kwa ujumla na ustawi wa raia, ni kidogo sana kusherehekea." "Hakuna pesa"

Moja ya vifungu vya makubaliano ya amani yanataka kurejeshwa nyumbani kwa wakimbizi wa ndani na wan je ya nchi.

"Serikali italazimika kuchangia pesa kwa ajili ya makazi mapya ya watu katika makazi yao, lakini inasema hakuna fedha," anaongeza Profesa Madut.

Ukosefu wa rasilimali pia ulionekana wakati wanatafuta chanjo dhidi ya covid-19, ni moja ya nchi changa zaidi duniani ambazo zimechanja watu wachache zaidi.

Katikati ya mwezi Disemba, Shirika la Afya Duniani (WHO) liliripoti kuwa Sudan Kusini imepokea jumla ya dozi zaidi ya nusu milioni ya chanjo ya anticovid, kwa nchi yenye wakazi milioni 11.

Lakini karibu nusu ya dozi bado hazijatumika, na hadi mwisho wa 2021 chini ya 2% ya Wasudan Kusini ndio walichanjwa.

Wakati huo huo, Emmanuel, ambaye alipoteza kila kitu katika vita, ikiwa ni pamoja na shamba lake na kaka yake, ambaye anasema "aliuawa" anaomba kwa serikali ya kitaifa, mamlaka ya serikali na "pengine jumuiya ya kimataifa" washirikiane "kuleta maisha yenye amani ya kudumu kwa watu wa Tambura na Ikweta Magharibi.

Anasema, kwanza lazima waondoe vikundi vyenye silaha kutoka msituni, kisha wanyang'anye idadi ya watu silaha na kuhimiza mazungumzo kati ya vikundi tofauti.

"Msaada zaidi wa kibinadamu unahitajika pia, kusaidia wenyeji kuondokana na majeraha ya kisaikolojia yaliyotokana na vita na kukarabati shule ambazo ziliharibiwa," anaendelea.

Kwa upande wake, Profesa Madut anapendekeza kuwa kuboreshwa kwa mfumo wa mahakama kunaweza kuwa hatua nzuri ya kumaliza mzozo huo.

Wanawake wazidi kuikimbia Sudan kusini

"Kwa sasa kulipiza kisasi ndio njia pekee ya kupata haki, kwa hivyo vurugu zinaendelea," anafafanua.

"Ikiwa hakuna dola inayotoa haki kwa watu waliodhulumiwa, watu daima watachukua njia ya kulipiza kisasi."

Chanzo: BBC Swahili