Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yaonyesha jeuri ya fedha Ethiopia, yaelekea DR Congo

Simba Kufuru Pic Data Simba yaonyesha jeuri ya fedha Ethiopia, yaelekea DR Congo

Wed, 10 Feb 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Thobias SebastianMore by this Author Msafara wa Simba leo umeendelea na safari ya kuelekea Kinshasa, DR Congo kwa ajili ya kuivaa AS Vita keshokutwa Ijumaa lakini kabla ya hilo, jana usiku ilitikisa Ethiopia ilikoweka kituo kwa muda jana ikitokea Tanzania kwa kuonyesha nguvu ya fedha iliyonayo mara baada ya kutua majira ya saa 1.25 usiku.

Iko hivi,msafara huo wa Simba mara baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole ulioko Addis Ababa, Ethiopia ulilala katika Hoteli ya Kifahari ya hadhi ya nyota tano ya Tulip iliyopo umbali wa takribani Kilomita tano kutoka katika uwanja huo wa Ndege wa Kimataifa wa Ethiopia.

Baada ya wachezaji, maofisa wa benchi la ufundi na viongozi wa Simba kupumzika ndani ya Hoteli hiyo, msafara huo leo asubuhi umeondoka kuelekea Kinshasa, safari iliyoanza saa 4.00 asubuhi huku wakitarajiwa kufika huko Saa 8.25 mchana.

Simba iliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Bole mnamo saa 2:00 asubuhi kisha kuanza kufanya ukaguzi na baadaye kuelekea katika geti 14A, ili kuunganisha ndege.

Mara baada ya kumaliza ukaguzi wote walifika katika eneo la geti 14A, na kukaa kusubiria ndege ya kuwapeleka Kinshasa.

Kocha wa viungo wa Simba, Adel Zrane mara baada ya kufika uwanja wa ndege wa Eithiopia alisema leo ni siku nzuri kwao na wachezaji wote waneamka salama kwa ajili ya safari.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz