Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba wazua taharuki Msumbiji

Simba Wazua Taharuki Msumbiji Simba wazua taharuki Msumbiji

Fri, 11 Nov 2022 Chanzo: Bbc

Simba, ambao wanadhaniwa kuwa walitoroka kutoka katika shamba moja nchini Msumbiji, wamesababisha wasi wasi na mkanganyiko katika vijiji vya Moamba vilivyopo katika jimbo la Maputo nchini Msumbiji.

Simba hao wamewauwa mifugo ya wanavijiji –jambo ambalo limekuwa likifanywa pia na fisi tangu mwanzoni mwa mwaka huu ambao waliwaua mbuzi na kondoo nyakati za usiku.

Katika kipindi cha siku 15 pekee, zaidi ya mifugo 20 wameuawa na kuliwa na simba.

Wanavijiji wanalalamika kwamba mamlaka hazifanyi lolote kuhusu suala hili, na simba wanaweza kuanza kuwashambulia binadamu.

Chanzo: Bbc