Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba aliyepotea kwa miaka 19 aonekana

Simba Mnyama Ers Simba aliyepotea kwa miaka 19 aonekana

Wed, 26 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba mkubwa aliyetoweka miaka 19 iliyopita katika Hifadhi ya Taifa ya Sena Oura nchini Chad ameoneka, ambapo mara ya mwisho alionekana katika hifadhi hiyo mwaka 2004.

Picha ya simba jike ilitolewa na timu ya wahifadhi kutoka Serikali ya Chad na Jumuiya ya Uhifadhi wa Wanyamapori ((WCS) yenye makao makuu yake mjini New York, Marekani hivi karibuni ambayo ilibaini simba huyo ndiye aliyetoweka miaka 19 iliyopita.

“Nina hakika hayuko peke yake,” Amesema Mkurugenzi Mtendaji wa WCS – Big Cat Programme, Luke Hunter .Picha hiyo iliyochukuliwa na kamera ya mbali katika eneo lililohifadhiwa mwezi Februari mwaka huu ilitolewa Alhamisi wiki iliyopita.

“Hii inatia moyo sana kwa sababu majike wakuu ndio msingi wa Simba wowote, na sio wazururaji wakubwa: wanakaa katika maeneo ambayo wana mawindo na wako salama kulea watoto wao,” Amesema Dkt. Hunter.

Mwaka 2014, Muungano wa Kimataifa wa Uhifadhi wa Viumbe Vilivyo Hatarini ulisema Simba wametoweka katika hifadhi ya Sena Oura.

Dkt. Hunter amesema kuna Simba kati ya elfu 22 na elfu 24 waliosalia porini, wengi wao wameainishwa kama jamii ndogo ya Simba wa Kusini Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live