Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba, Zamalek na kifo cha Foe halikurudi

Zamaleck Pic Data Simba, Zamalek na kifo cha Foe halikurudi

Tue, 9 Feb 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

Katika miaka ambayo siwezi kuisahau, ni wakati ule nikiwa Mhariri wa Habari wa Mwanaspoti, mwanzoni mwa miaka ya 2000.

Mwanaspoti hasa lengo lake lilikuwa kuandika habari za michezo ambazo hazipewi nafasi sana kwenye vyombo vya habari vingine na kama vikipata nafasi basi hata jinsi ya kuripoti ni kwa kiasi kidogo.

Michezo ambayo haikuwa ikipata nafasi ni kama netiboli, skwashi, gofu, na mingine mingi iliyokuwa ikichezwa uswahilini, ligi mbalimbali na hapo ndipo Mwanaspoti lilipopata umaarufu, na mfano mzuri mashindano ya Lucky Rangers yaliyokuwa yakifanyika Mwananyamala.

Mwanaspoti ni kati ya magazeti yaliyoyabeba mashindano yale ambayo baadaye yalikuja kupata udhamini, lakini ni kutokana na moto wake na jinsi Mwanaspoti lilivyokuwa likiyapa umuhimu pamoja na mashindano mengine. Pamoja na matukio hayo, Mwanaspoti lilikuwa likiripoti pia mechi za kitaifa na kimataifa.

Mwaka 2003 kulikuwa na matukio mengi ya michezo, lakini mawili ninayoyakumbuka ni yale yaliyorudisha nakala sifuri.

Tukio mojawapo ni la Simba kuivua ubingwa wa Afrika, Zamalek ya Misri. Mwanaspoti lilisubiri mchezo ule uliopigwa usiku ambao Simba iliyokuwa chini ya kocha marehemu, James Aggrey Siang’a walifanyiwa kila aina ya vitimbi ukichukulia Simba ilishinda mchezo wa kwanza Dar es Salaam 1-0.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz