Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sijutii uamuzi wa kujaribu kuchelewesha uchaguzi wa Senegal: Sall

Sijutii Uamuzi Wa Kujaribu Kuchelewesha Uchaguzi Wa Senegal: Sall Sijutii uamuzi wa kujaribu kuchelewesha uchaguzi wa Senegal: Sall

Wed, 20 Mar 2024 Chanzo: Bbc

Rais wa Senegal Macky Sall amesema kuwa hajutii jaribio lake la kuahirisha uchaguzi ambao ulipaswa kufanywa mwezi uliopita, na kusababisha maandamano mabaya nchini humo.

Katika mahojiano na BBC, Bw Sall alisema kuwa uamuzi wa kucheleweshwa kwa uchaguzi huo haukuchukuliwa upande mmoja, bali ulitokana na wasiwasi wa uchaguzi uliotolewa na wabunge."

Sina msamaha wa kuomba, sijafanya kosa lolote. Ninazungumza na wewe kama rais wa jamhuri.

Hatua zote zilizochukuliwa zimekuwa ndani ya mfumo wa sheria na kanuni," Rais Sall alisema.

Mipango yake ya kuchelewesha uchaguzi, ambayo ilisababisha mapigano makali na mvutano wa kisiasa kote nchini, hatimaye ilibatilishwa na mahakama kuu ya nchi.

Uchaguzi huo unatazamiwa kufanyika Jumapili baada ya kushindwa kwa jitihada za kuusukuma hadi Desemba.

Wakosoaji walikuwa wamemshutumu rais kwa kujaribu kuongeza muda wake wa kukaa madarakani.

Lakini Bw Sall anasisitiza kwamba hatakaa siku moja zaidi hata kama kura ya Jumapili haitatoa mshindi wa moja kwa moja.

Wiki iliyopita, kiongozi mkuu wa upinzani na mmoja wa wakosoaji vikali wa Bw Sall Ousmane Sonko na mgombeaji urais wa chama chake Bassirou Diomaye Faye waliachiliwa kutoka gerezani chini ya msamaha wa rais.

Rais Sall anakanusha kuwa mashtaka dhidi ya wapinzani wake yalichochewa kisiasa.Anaachia madaraka baada ya kuhudumu kwa mihula miwili.

Chama chake tawala cha muungano Benno Bokk Yakaar (BBY) kimemchagua Amadou Ba mwenye umri wa miaka 62 kuwania kiti cha urais.

Chanzo: Bbc