Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sibanda: Natamani viongozi wote wa Afrika wafuate nyayo za JPM

F0515405e21c6c80b484aa6d00d3b457 Sibanda: Natamani viongozi wote wa Afrika wafuate nyayo za JPM

Sun, 7 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WAKILI kutoka nchini Afrika Kusini, Sabelo Sibanda alisema wanaitazama Tanzania kama kilelezo cha Uhuru na jukwaa la utambulisho wa waafrika na kudai kuwa anatamani viongozi wote wa Afrika wawe na maono kama ya Rais John Magufuli katika kukabiliana na janga la virusi vya Corona.

Akizungumza katika kongamano la kujadili Umuhimu wa Umajumui wa Afrika katika kutatua changamoto na fursa zinazosababishwa na Covid -19 lililofanyika leo jijini Dar es Salaam, alisema Bara la Afrika linatakiwa kutafuta utaratibu wake wa namna ya kushughulika na Virusi vya Corona na sio kupangiwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Alisema anatamani viongozi wote Afrika wangekuwa na maono kama ya Rais John Magufuli ya kuthamini juhudi za ndani kabla ya kusaka suluhu ya matatizo yao nje.

Alisema Tanzania imetoka katika kipindi cha kuelekezwa na kupangiwa cha kufanya na hivi sasa inatoa ujumbe mzuri katika bara la Afrika kuwa inaweza kujipangia cha kufanya na haielekezwi na taifa lolote.

“Afrika ya kesho inajengwa leo hakuna haja ya mataifa ya Afrika na dunia kuisema Tanzania kwa sababu anachofanya Magufuli ni kuijenga Tanzania ya kesho kwa kuanza na kuweka mipango hiyo leo,” alisema Wakili Sibanda.

Sibanda alisema lengo la mataifa ya Magharibi ni kuona mataifa ya Afrika yanaharibikiwa ndio maana yaliweka mipaka katika ardhi ya Bara hilo ili kutenganisha watu wake na kuzuia jaribio lolote la kuifanya Afrika kuwa nchi moja.

“Ukiangalia Tanzania sasa hivi ni nchi ya kupigiwa mfano Afrika kwa kuthamini rasilimali zake kuanzia madini, utalii, miundombinu na watu wake,” alisema Sibanda.

Chanzo: www.habarileo.co.tz