Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shule iliyosababisha vifo vya wanafunzi yafungwa

94531 Pic+shule Shule iliyosababisha vifo vya wanafunzi yafungwa

Wed, 5 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kakamega. Wizara ya Elimu nchini Kenya imetanga kuifunga shule ya msingi Kakamega baada ya watoto 15 kupoteza maisha.

Waziri wa Elimu, George Magoha alisema Serikali imeamua kufunga shule hiyo ili kuruhusu uchunguzi wa tukio hilo.

Wanafunzi hao walipoteza maisha juzi Jumanne iliyopita Februari 3, baada ya kukanyagana walipokuwa wakijaribu kujiokoa na dharura.

Mkanyagano huo ulitokea wakati wanafunzi saa 11 jioni baada ya kengele ya dharura kupigwa na kusababisha wanafunzi kukimbia ovyo ili kujiokoa ambako wengine waliruka kutoka ghorofani.

Waziri Magoha alisema kuwa wavulana watano na wasichana tisa walifariki katika mkasa huo.

Hata hivyo, waziri Magoha alisema mpaka sasa chanzo cha tukio hilo hakijajulikana na maafisa wa usalama wanaendelea na uchunguzi.

Pia Soma

Advertisement
Awali Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Kakamega, David Kabena alisema wanafunzi wengine 39 walijeruhiwa katika tukio hilo.

Chanzo: mwananchi.co.tz