Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shughuli ya uokoaji inaendelea baada ya moto kuibuka katika soko Somalia

Shughuli Ya Uokoaji Inaendelea Baada Ya Moto Kuibuka Katika Soko Somalia Shughuli ya uokoaji inaendelea baada ya moto kuibuka katika soko Somalia

Sun, 10 Mar 2024 Chanzo: Bbc

Wazima moto nchini Somalia wamekuwa wakishirikiana na polisi na raia katika juhudi za kuuzima moto mkubwa ambao umezuka mapema Jumapili katika soko la Bakara mjini Mogadishu.

Moto huo mkubwa unaoripotiwa kuanza mapema asubuhi, umeteketeza maduka kwenye soko hilo kubwa kabisa mjini Mogadishu ambalo ni mashuhuri kwa wafanyibiashara wa bidhaa mbali mbali na wanunuzi.

Wengi waliofika kuanza shughuli zao za mwanzo wa wiki baada ya mapumziko ya wikendi, walipatwa na mshtuko kuuona moto ukisambaa kwa haraka.

Polisi nchini humo wamesema kwamba pindi tu, moto utakapo dhibitiwa, uchunguzi kujuwa chanzo cha moto huo utaanzishwa mara moja.

Chanzo: Bbc