Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shirika la ndege la Qatar kushitakiwa unyanyasaji wa kijinsia

Qatar Pix Shirika la ndege la Qatar kushitakiwa unyanyasaji wa kijinsia

Mon, 15 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kundi la wanawake waliofanyiwa vipimo vya lazima vya uzazi katika uwanja wa ndege wa Doha wamejipanga kufungua mashtaka dhidi ya Mamalaka za Qatar kwa madai kuwa walifanyiwa vitendo vilivyo kinyume na haki za binaamu.

Wakili, Damian Sturzaker, anayetarajiwa kuwatetea katika kesi hiyo amewaambia waandishi wa habari kuwa wanawake hao 10 walikuwa wakisafiri na ndege ya Qatar kutoka Doha, wakiwemo raia 13 wa Austaria walilazimika kufanyiwa vipimo hivyo wakati Mamalaka za mjini hapo zikiwa kwenye zoezi la kumtafta mama aliyetelekeza mtoto katika maliwato ya uwanja huo wa ndege.

Tukio hilo limelalamikiwa na wadau wa haki za binadamu kutoka sehemu tofauti duniani huku wengi wakihoji juu ya usalama wa wageni watakao fikia nchini humo kwa ajili ya kufuatilia, kushiriki kombe la dunia linalotarajiwa kufanyika mwaka 2022.

Wakili huyo kutoka jiji la Sydney nchini Austaria amesema kuwa wanawake saba kati ya waliofanyiwa vipimo hivyo kwa lazima wamepata athari za kiafya jambo lililomsukuma kutuma ujumbe kwa Mamlaka za Qatar.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live