Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shirika la ndege la Nigeria laomba radhi kwa kutua kimakosa

Shirika La Ndege La Nigeria Laomba Radhi Kwa Kutua Kimakosa Shirika la ndege la Nigeria laomba radhi kwa kutua kimakosa

Mon, 27 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Shirika la ndege la Nigeria limeomba radhi kwa "kutokuelewana" baada ya abiria kuambiwa wamefika mahali wanakokwenda, Abuja, wakati walikuwa wametua zaidi ya kilomita 450 (maili 280) katika mji mwingine wa Asaba.

Shirika la ndege la United Nigeria lilisema safari ya ndege ya Jumapili kutoka jiji kuu la Lagos hadi mji mkuu, Abuja, ilielekezwa kwa muda hadi Asaba katika jimbo la Delta, kutokana na hali mbaya ya hewa.

Ilisema kuwa tangazo lisilo sahihi lilitolewa kwa abiria wakati ndege hiyo ilipotua Asaba, na kusababisha mkanganyiko.

"Baada ya kuwasili, wahudumu walitangaza kwa ujasiri kwamba tumefika Abuja, tulibaini kuwa tumefika Asaba," msafiri alisema kwenye ukurasa wa X, akiongeza kuwa "inavyoonekana, rubani wetu alipewa mpango ndege wa tofauti kutoka Lagos".

Lakini shirika hilo la ndege lilisema rubani wa ndege hiyo alikuwa anafahamu kuhusu mabadiliko hayo na alifahamishwa ipasavyo. "Tunaomba radhi kwa kutoelewana kwenye ndege yetu. Kwa sasa tunachukua hatua kuzuia matukio kama hayo katika siku zijazo,” ilisema taarifa. Taarifa ilisema ndege hiyo hatimaye ilitua salama Abuja.

Chanzo: Bbc