Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shirika la ndege la Kenya kulipa mafao ya wafanyakazi

Shirika La Ndege La Kenya Kulipa Mafao Ya Wafanyakazi Shirika la ndege la Kenya kulipa mafao ya wafanyakazi

Fri, 24 Feb 2023 Chanzo: Voa

Shirika la ndege la Kenya litaanzisha upya kuwasilisha michango ya kila mwezi ya wafanyakazi wake kwa mfuko wa pensheni ambayo ilisimamishwa kutokana na janga la COVID.

Barua ya ndani ya shirika hilo ilionyesha Alhamisi kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, ikidai shirika hilo kusuluhisha malalamiko makubwa yaliyosababisha mgomo wa marubani.

Mwezi Novemba mwaka jana, maelfu ya abiria walikwama kufuatia mgomo wa marubani 400 walilitaka shirika hilo lianze kuchangia mafao yao na kutatua tatizo la malipo yaliyo kuwa yameahirishwa. Mgomo huo ulimalizika baada ya amri ya mahakama.

Shirika hilo, ni moja ya makampuni makubwa barani Afrika, limesema katika taarifa yake kuwa halina budi kulipa malimbikizo yote tangu mpango huo ulipositishwa mwezi Machi 2020.

Hatua hiyo inafuatia tathimini ya shirika hilo la ndege likisema “utekelezaji wa uboreshaji unaoendelea” taarifa ambayo imetiwa saini na mkuu wa idara ya wafanyakazi. Hakuna majibu yalitolewa kwa haraka na utawala la shirika hilo la ndege kuhusu taarifa hio.

Serikali inaliona shirika la ndege la Kenya kuwa muhimu kwa shuguli za utalii na kiuchumi kwa ujumla kutokana na jukumu lake la usafiri, lakini kwa miaka ya hivi karibuni limekuwa likipata hasara ambayo imelisukuma kushindwa kumudu matengenezo ya kiufundi

Chanzo: Voa