Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shirika la ndege la Ethiopia limekanusha madai ya kusafirisha silaha bila kibali

Ethipia2 Shirika la ndege la Ethiopia lakanusha madai ya kusafirisha silaha bila kibali

Tue, 7 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la ndege la Ethiopia limekanusha madai ya kusafirisha silaha nchini Sudan kinyume na taratibu, kwa kusema kuwa madai hayo hayan aukweli kwani walifuata taratibu zaote za usafirishaji silaha.

Awali taarifa ya madai hayo ilitolewa na moja ya kituo cha habari na mawasiliano cha nchini Sudan kinachoitwa SUNA news Agency,kikilishtumu shirika hilo kwa kusafirisha siaha hizo ambazo zilikamatwa na mamlaka za usafiri wa anga nchini humo.

Taarifa ilieeza kuwa ndege hiyo ya abiria iliyosafiri kutoka mji mkuu wa Addis Ababa, kuelekea Khartoum ilikuwa na maboksi 72 ya silaha yaliyo kamtwa na mamlaka ya usafiri wa anga nchini Sudan.

" Bila kibali maalum, Mamlaka ya usafiri wa anga katika mji wa Addis Ababa uliiruhusu ndege hii kutoka hapo kuja hadi Khartoum ikiwa imebeba silaha ambazo zinahisiwa kuwa ni maalum kwa ajili ya kufanya uhalifu dhidi ya Serikali, ikiwa ni pamoja nakuvunja amani. Imesema taarifa hiyo.

Hata hivyo uongozi wa Shirikia hilo la ndege umekanusha vikali tuhuma hizo na kusema kuwa walisafirisha silaha hizo kwa kibali maalum

Chanzo: www.tanzaniaweb.live