Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shirika la ndege Kenya laingia mkataba na Congo kusafirisha mizigo

Kenya Airways22 Shirika la ndege la Kenya lakodisha ndege kwa Kongo kusafirisha mizigo

Tue, 14 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikala ndege la nchini Kenya (KQ), limekodisha ndege mbili kwa shirika la ndege la nchini Congo kwa makubaliano maalumu ya usafirishaji wa shehena .

Mkataba huo unaojumuisha ndege za Embraer E190, unakuja wakati KQ ikiwa imeanzisha safari za moja kwa moja za kusafirisha mizigo kati ya Johannesburg, Afrika Kusini na Lumbashi mji wa tatu kwa ukubwa nchini Congo.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa kitengo cha Usafirishaji mizigo cha KQ, Allan Kilavuka, amesema ndege za mizigo zilikuwa katika mpango wa kukuza zabuni za shirika hilo, huku wakiwa wameweka malengo ya kuongeza usafirishaji kwa asilimia 20 kutoka asilimia 7 za sasa.

"KQ ndio kitovu kikuu cha usafiri wa anga barani Afrika, ukijumuisha kuwa shirika hili lina uzoefu wa miaka 40, hatua hii ni muhimu katika kuimarisha ushirikiano ikiwa ni pamoja na kuongeza muungano wa amasuala ya anga, lakini pia kuwapa abiria nafasi ya kuchagua wapi watume mizigo yao"-Bwana Kilavuka

Chanzo: www.tanzaniaweb.live