Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shirika la misaada lakata rufaa kuhusu wahamiaji wa Rwanda

E9dfd1c1 1a91 4f15 B35a 42e0f237487f Shirika la misaada lakata rufaa kuhusu wahamiaji wa Rwanda

Mon, 16 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la misaada la Uingereza Jumatatu asubuhi litaomba kibali kutoka kwa Mahakama Kuu mjini London kukata rufaa dhidi ya mpango tata wa serikali wa kutuma baadhi ya waomba hifadhi nchini Rwanda.

Shirika hilo la msaada kwa wahamiaji litahoji kuhusu mahakama "kukosea" katika uamuzi wake wa mwezi Disemba kuhusu mpango huo kuwa halali na itapinga uamuzi kuwa nchi hiyo ni mahali salama kwa wahamiaji.

Ikiwa mahakama itaruhusu rufaa ya shirika la msaada, safari zote za ndege chini ya mpango huo zitacheleweshwa zaidi. Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak na Waziri wa Mambo ya Ndani Suella Braverman wamefanya kuzuia uhamiaji kwa kipaumbele cha kisiasa.

Mnamo mwezi Disemba Mahakama Kuu ilikubali uamuzi wa serikali na kupunguza haki za wahamiaji kupinga maamuzi ya kuwapandisha ndege kurudi kwao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live