Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shirika la Usimamizi wa Afya Afrika latupa lawama kwa Umoja wa Mataifa kwa kuzinyima nchi maskini chanjo

ADC AFRIKA CDC Afrika lawatupia lawama viongozi umoja wa mataifa kwa uhaba wa chanjo

Fri, 10 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la usimamizi wa Afya la Umoja wa Afrika limewatupia lawama viongozi wa Umoja wa Mataifa kwa kushindwa kutoa chanjo ya UVIKO-19 kwa nchi maskini, jambo ambalo limepelekea kuongeza kasi ya kusambaa kwa viriusi hivyo katika mataifa hayo.

Shrika hilo limeeleza kuwa takribani asilimia 3.18 ya watu wamepokea chanjo hiyo kiwango ambacho wamekitaja kuwa ni hafifu kwa kulinganisha na idadi ya watu barani humu ambayo ni bilioni 1.3.

"Hatuwezi kuendelea kupiga siasa katika jambo hili, kuendelea kuweka malengo ambayo hayafikiki kwa jinsi yoyote ni kupoteza muda, ahadi hazitatuleta chanjo mikononi"-imesema taarifa ya shirika hilo.

Hata wamezisistiza nchi za Afrika kujitahidi kuwaelemisha wananchi kujilinda dhidi ya virusi hivi kwa kufuata tahadhari ziliwekwa na Shirika la Afya Duniani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live