Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shirika la Ndege Uganda laingiza bilioni 40/-

09e18e10dfd8d4eb2212ca543607d620.png Shirika la Ndege Uganda laingiza bilioni 40/-

Tue, 16 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

SHIRIKA la Ndege la Uganda limepata mapato yenye thamani ya Sh bilioni 40 tangu lilipoanza kufanya kazi hadi mwisho wa Desemba, mwaka jana.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa shirika hilo, Cornwell Muleya amesema ndege za shirika hilo zilibeba abiria 77,355 kati ya Agosti, 2019 na Juni, 2020, ikiwa ni upungufu wa asilimia 10 kutoka kwa lengo la abiria 85,760.

Hiyo ina maanisha kuwa lengo la mapato walilojiwekea ya Sh bilioni 31.5 halikufikiwa na badala yake lilizalisha Sh bilioni 25.2.

Shirika hilo lilifanya nyongeza ya Sh bilioni 14.8 kutoka kwa abiria 26,394 mwishoni mwa Desemba, mwaka jana.

Kiwango cha wastani cha mizigo wa abiria kwa kipindi cha kwanza kilikuwa asilimia 35 lakini baadaye kiliongezeka hadi asilimia 47 wakati sekta ilijitahidi kukabiliana na athari ya janga la covid-19.

Muleya aliiambia Kamati ya Miundombinu ya Bunge kuwa shughuli za kibiashara za shirika hilo la ndege zilisitishwa Machi, mwaka jana hadi Juni, mwaka jana kabla ya kufungua tena safari za ndege za kibiashara kwani anga bado ilikuwa imefungwa.

Lakini baada ya kuanza tena kazi Oktoba, shirika hilo lilifanikiwa kufanya kazi katika maeneo tisa ikiwamo kwenda Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Sehemu nyingine ni Bujumbura, Burundi, Nairobi na Mombasa nchini Kenya, Mogadishu nchini Somalia, Juba, Sudan Kusini, Dar es Salaam, Zanzibar na Arusha, Tanzania.

Shirika la Ndege la Uganda limepanga kuanza safari za njia ndefu kwenda Guangzhou nchini China, London nchini Uingereza, Mumbai nchini India na Dubai katika Falme za Kiarabu mwezi ujao.

Chanzo: habarileo.co.tz