Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shirika la Kenya lakanusha kumuajiri mtangazaji wa televisheni

Shirika La Kenya Lakanusha Kumuajiri Mtangazaji Wa Televisheni Shirika la Kenya lakanusha kumuajiri mtangazaji wa televisheni

Thu, 14 Mar 2024 Chanzo: Bbc

Shirika linalosimamia uteuzi wa watu nchini Kenya limekanusha ripoti kwamba lilimuajiri mtangazaji maarufu wa zamani wa televisheni ambaye hivi majuzi aliachiliwa kwa kosa la mauaji.

Waziri wa Utumishi wa Umma Moses Kuria wikendi iliyopita aliambia tovuti ya kibinafsi ya Nation kwamba Tume ya Utumishi wa Umma (PSC) ilimteua mtangazaji wa zamani wa televisheni Jacque Maribe kuwa mkuu wa mawasiliano katika wizara yake.

Tangazo hilo lilizua ukosoaji mkubwa kwenye mitandao ya kijamii huku maswali yakiibuka kuhusu iwapo uteuzi wa Bi Maribe ulifuata utaratibu ufaao wa kuajiri.

PSC mnamo Alhamisi ilikanusha madai ya Bw Kuria, ikisema kuwa haijamteua Bi Maribe wala kupokea ombi la kumwajiri.

"Kwa rekodi, nafasi iliyotajwa itajazwa kupitia mchakato wa ushindani iwapo nafasi itatokea," mwenyekiti wa PSC

Anthony Muchiri alisema katika taarifa hiyo iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Bi Maribe mwezi uliopita aliondolewa hatia ya kumuua mfanyabiashara Monica Kimani baada ya kesi ya miaka sita.

Yeye na aliyekuwa mchumba wake Joseph Irungu, ambaye pia anajulikana kama "Jowie", walikuwa wameshtakiwa kwa mauaji ya mfanyabiashara huyo, ambaye alipatikana akiwa amekatwa koo katika nyumba yake jijini Nairobi mnamo 2018.

Irungu alihukumiwa kifo siku ya Jumatano baada ya mahakama kumpata na hatia ya mauaji hayo.

Chanzo: Bbc