Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shinikizo laongezeka kwa Rais Ruto kutangaza dharura ya kitaifa

Shinikizo Laongezeka Kwa Rais Ruto Kutangaza Dharura Ya Kitaifa Shinikizo laongezeka kwa Rais Ruto kutangaza dharura ya kitaifa

Wed, 1 Mar 2023 Chanzo: Voa

Shinikizo linaongezeka kwa Rais wa Kenya William Ruto kutangaza dharura ya kitaifa juu ya rekodi mbaya ya ukame katika nchi hiyo hasa upande wa kaskazini mwa nchi ambapo takriban watu milioni tano wameathiriwa.

Mvua kutonyesha kwa msimu wa sita mfululizo kunafanya hali ya njaa kuwa mbaya sana kote katika eneo hilo. Kaunti ya Wajiri, ndiyo imekumbwa vibaya na ukame ambako zaidi ya nusu ya watu huko wanakabiliwa na ukosefu wa usalama wa chakula.

Waathirika wa ukame katika maeneo yaliyokumbwa na ukame wanasubiri kwa hamu misaada katika kijiji cha Kilkiley kwenye Kaunti ya Wajiri. Maelfu ya wafugaji wameweka kambi barabarani ili kutafuta misaada kutoka katika magari yanayopita njiani na makundi ya misaada, akiwemo Rukia Ahmed. Anatengeneza chai kwa ajili ya watoto wake anasema “hatuna chochote cha kupika hivi sasa. Tuko hapa ili kupata msaada, NGOs au watu wanaopita.”

Mamlaka nchini Kenya zinasema mvua kutonyesha kwa msimu wa sita mfululizo kumesababisha mamilioni ya mifugo kufa na kuwaacha Wakenya takriban milioni tano wakihitaji misaada ya kibinadamu.

Zaidi ya nusu ya wale walioathiriwa wako katika kaunti tatu za kaskazini mashariki mwa Kenya – Garissa, Wajir na Mandera.

Chanzo: Voa