Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sheria ya ushoga yaanza kazi Uganda

Rais Museveni: Sheria ya ushoga yaanza kazi Uganda

Tue, 29 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 20 amekuwa raia wa kwanza nchini Uganda kuhukumiwa chini ya sheria mpya ambapo kosa la ushoga uliokithiri hupewa adhabu ya kifo.

Kwa mujibu wa nyaraka ambazo zilionwa na shirika la habari la Reuters, Mwanaume huyo aliyehukumiwa Agosti 18 alikutwa na kosa la kufanya mapenzi yasiyokubalika kisheria na mwanaume mwenye umri wa miaka 41.

Hata hivyo nyaraka hizo hazikueleza sababu iliyopelekea kosa lake kuwekwa kwenye kundi la "ushoga uliokithiri".

Mwanasheria wa mwanaume huyo Bi.Justine Balya amesema kuwa anaamini sheria hiyo nzima ipo kinyume na katiba.

"Malalamiko juu ya hii sheria yalikwishawasilishwa mahakamani lakini majaji bado hawajaisikiliza hii kesi "

Bi. Balya amesema kuwa hadi sasa anafahamu watu wanne ambao wameshtakiwa chini ya sheria hiyo, hata hivyo mteja wake ndiye wa kwanza kuhukumiwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live