Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shekhe: Waislamu wanasoma sana magazeti kuliko Quran

Tachomwa Quaran Shekhe: Waislamu wanasoma sana magazeti kuliko Quran

Thu, 5 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waumini wa Dini ya Kiislamu katika mkoa wa Kilimanjaro wamekumbushwa kujenga utaratibu kwa vijana wao kusoma kitabu kitakatifu cha Quran sambamba na kutoa hamasa kwa wale wenye nia ya kuhifadhi Quran.

Hayo yameelezwa na Sheakh Mkuu wa wilaya ya Moshi wakati wa mashindano ya uosomaji wa Quran tukufu,mashindano yaliyofanyika katika msikiti wa Shia na kushirikisha zaidi ya vijana 40 kutoka Madrasa mbalimbali za Manispaa ya Moshi.

Taasisi ya Bilal Muslim Mission Tanzania inawakutanisha waumini wa Dini ya Kiislamu katika Msikiti wa Shia uliopo katikati ya mji wa Moshi,lengo likiwa ni vijana kuoneshana uwezo wa kuhifadhi kitabu kitakatifu cha Quran katika mashindano yaliyobeba kauli mbiu ya Elimu ni Muhimu kwa kila Binadamu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live