Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shambulizi la Al Shabab ladhibitiwa Kenya

90865 Pic+shabab Shambulizi la Al Shabab ladhibitiwa Kenya

Sun, 5 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

NAIROBI, Kenya. Kundi la kigaidi la Al Shabab limejinadi kufanya shambulio katika kambi ya kijeshi nchini Kenya inayotumiwa na wanajeshi wa Kenya na Marekani.

Katika taarifa yake kundi hilo lilijinadi kufanya shambulio hilo katika kambi hiyo iliyokuwa Kusini Mashariki mwa Kenya lakini taarifa zinadai kwamba shambulio hilo lilidhibitiwa.

“Kuna shambulio limefanywa lakini limedhibitiwa,'' alisema  Irungu Macharia, ofisa wa Serikali mjini Lamu ilipo kambi hiyo. Hata hivyo Macharia hakusema kama kuna madhara yoyote ya kibinadamu au uharibifu wa mali uliotokea.

Katika taarifa ya Jeshi la Ulinzi la Kenya ilielezwa kwamba magaidi wanne waliuawa na kwamba mpango wa magaidi hao haukufanikiwa.

Taarifa ya kambi ya kijeshi ya Marekani barani Afrika ilieleza kulijua tukio hilo lakini taarifa hiyo haikueleza kwa mapana undani wa tukio zima.

Al Shabab ni kundi la kigaidi linalosifika kwa kufanya mashambulizi ya kigaidi maeneo mbalimbali hasa kwa Marekani na washirika wake duniani kote

Chanzo: mwananchi.co.tz