Idadi vifo vilivyotokana na mashambulizi dhidi ya watu vijijini, yaliyofanywa na wanamgambo jimboni Ituri la kaskazini-mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo – DRC, iliongezeka kutoka watu 15 hadi kufikia 41, wakiwemo wanawake na watoto.
Wanamgambo wa jumuiya ya Cooperative for the Development of Congo – CODECO, ambao wanadai kulinda kabila la Lendu dhidi ya kabila la Hema, wanatuhumiwa kutekeleza mashambulizi mapema Jumamosi asubuhi dhidi ya vijiji vitano katika eneo la Mahagi, kuua wakazi, kuiba ng’ombe, uporaji na kuchoma nyumba.
Mkuu wa utawala wa Panduru, ambako vijiji vilivyolengwa vinapatikana, Arnold Lokwa alisema miili ya wahasiriwa 15 imepatikana mingi ikiwa ni wanawake, watoto na wazee huku akibainisha kuwa, “sasa tumekufa 31na msako unaendelea na bado mashambulizi yanaweza kuongezeka.”
Amesema, “tayari tumekusanya miili 39,” kilisema chanzo cha kibinadamu. “Wengi wa wahasiriwa ni wanawake” na angalau watoto wadogo watatu ni miongoni mwa waliokufa, maiti hawa 39 walipatikana katika vijiji vitatu, kupata vijiji vingine viwili bado haiwezekani kwa sababu za usalama.”
Jumamosi Machi 18, 2023, huko mashariki mwa DRC, katika jimbo jirani la Kivu Kaskazini, waasi wa Allied Democratic Forces – ADF, wenye mafungamano na kundi la wanajihadi la Islamic State – IS, wanatuhumiwa kuua takriban watu tisa katika kijiji cha Nguli, huko Lubero na IS ilidai kuhusika na shambulio hilo kama ambavyo lilikiri kuhusika na shambulio lililoua takriban watu 40 Machi 8, 2023.