Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shambulio la RSF laua watu 22 el-Fasher, magharibi mwa Sudan

Watu 123 Wamefariki Sudan Wiki Mbili Zilizopita; Inasema Shirika La Misaada Shambulio la RSF laua watu 22 el-Fasher, magharibi mwa Sudan

Mon, 29 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa akali watu 22 wameuawa katika shambulio linalodaiwa kufanywa na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) katika mji wa el-Fasher, jimboni Darfur, magharibi mwa Sudan.

Kamati ya Mapambano ya el-Fasher imesema katika taarifa iliyochapishwa jana kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook kuwa, wapiganaji wa RSF wameshambulia kwa maroketi masoko, hospitali na majengo ya makazi ya watu na kusababisha maafa hayo.

Imesema RSF imetumia pia droni katika hujuma dhidi ya hospitali moja mjini el-Fasher na kusababisha vifo vingi. Baadhi ya duru za habari zinasema kuwa, watu 97 wameuawa katika mashambulio hayo ya RSF. Hata hivyo viongozi wa Vikosi vya Msaada wa Haraka wamekanusha madai ya kuhusika na mashambulizi hayo ya umwagaji damu.

Hii ni katika hali ambayo, Ibrahim Khatir, Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya ya Jimbo la Darfur Kaskazini alisema karibuni kuwa, kwa mujibu wa rekodi rasmi, watu zaidi ya 600 wameuawa na takriban 4,500 wengine wamejeruhiwa huko el-Fasher tangu Mei 10 mwaka huu hadi sasa.

Wapiganaji wa RSF Wakati huo huo, kwa akali watu 12 wameripotiwa kuaga dunia kutokana na athari za mvua kubwa zinazonendelea kunyesha katika jimbo la Kassala, mashariki mwa Sudan.

Hayo yalisemwa jana na Haitham Mohamed Ibrahim, Waziri wa Afya wa Sudan na kuogeza kuwa, mvua kubwa inayonyesha huko mashariki mwa Sudan imezidisha mateso ya watu waliokimbia makazi yao haswa katika miji ya Gedaref, Kassala na Halfa Aj Jadeedah.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live