Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shambulio la ADF dhidi ya kanisa lasababisha vifo Kivu Kaskazini

Wansjeshi Butubd Fmdrcccc.jpeg Shambulio la ADF dhidi ya kanisa lasababisha vifo Kivu Kaskazini

Thu, 1 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu wanane waliuawa, wakiwemo watano kanisani, wakati wa shambulio lililotekelezwa Jumanne jioni mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na waasi wa ADF, wanaoshirikiana na kundi la Islamic State (IS), kulingana na shirika la habari la AFP likinukuuu vyanzo vya ndani.

Kulingana na vyanzo hivi, ADF (Allied Democratic Forces) walifanya uvamizi katika eneo la Baeti, karibu na mji wa Oicha, katika eneo la Beni katikamkoa wa Kivu Kaskazini, kwenye mpaka na Ituri. Mikoa yote miwili imekuwa chini ya hali ya kuzingirwa tangu 2021, hatua ambayo ilibadilisha mamlaka ya kiraia na utawala wa kijeshi ili kupambana na makundi yenye silaha.

"Miili minane ya raia waliouawa na ADF iliwekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti" cha hospitali ya Oicha, wakiwemo "Wakristo watano wa Kibranhamisti waliouawa katikati ya ibada" huko Baeti, Nicolas Kikuku, Mkuu wa wilaya ya Oicha, ameliambia shirika la habari la AFP. Maadui waliwaua,” amesisitiza na kuongeza kuwa watu wengine kadhaa hawajulikani walipo.

Darius Syahira, ripota wa mashirika ya kiraia ya eneo hilo, amethibitisha shambulio hilo na kubaini kwamba "miili" ilikuwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti, bila kutoa idadi sahihi. Kundi la ADF, waasi wa Uganda, limeanzishwa tangu katikati ya miaka ya 1990 mashariki mwa DRC, ambapo wameua maelfu ya raia. Mnamo mwaka 2019 walitangaza kuungana na ISIS, ambayo inachukulia waasi hao kama "tawi lake Afrika ya Kati" (ISCAP kwa Kiingereza).

Mwishoni mwa mwaka 2021, baada ya mashambulizi yaliyohusishwa na waasi hao katika ardhi ya Uganda, Kampala na Kinshasa zilianzisha operesheni ya pamoja ya kijeshi dhidi ya ADF, iliyoitwa "Shujaa", lakini waasi wanaendelea na vitendo vyao vya kikatili.

Mwezi Desemba, walishtakiwa kwa kuanzisha mashambulizi mawili magharibi mwa Uganda, ambapo wanakijiji 13 waliuawa. Nchini DRC, baada ya wiki za utulivu, mashambulizi mabaya yaliyohusishwa na ADF yalianza tena kwa wiki moja katika eneo la Beni. Mnamo Januari 23, raia watano waliuawa katika mji huo, katika shambulio lililodaiwa na ISCAP.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live