Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shahada za Kenya kupigwa marufuku Nigeria

Graduates Cover Small Shahada za Kenya kupigwa marufuku Nigeria

Thu, 4 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nigeria imesema huenda ikaziongeza nchi za Kenya na Uganda katika orodha ya nchi ambazo shahada zao vya vyuo vikuu hazitotambuliwa na nchi na nchi hiyo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Elimu wa Nchi hiyo, Tahir Mamman siku ya Jumatano, Januari 03, 2023, wakati akihojiwa katika kituo cha Televisheni cha Nigeria, ambapo pia amebainisha kuwa nchi hiyo imeanzisha uchunguzi rasmi kuhusu Wizara na mashirika yanayohusika na kuidhinisha vyeti vya masomo nje ya nchi.

Hatua hiyo imefuata ikiwa ni siku chache tu, baada ya nchi hiyo ya Afrika Magharibi kusitisha kuzitambua shahada kutoka nchi za Benin na Togo, hatua ambayo nayo ilitokana na baada ya Mwandishi mmoja wa Habari za Uchunguzi nchini humo, kufichua namna alivyopata shahada ya miaka minne kutoka katika chuo kikuu kimojawapo, kilichopo katika Jamhuri ya Benin, ndani ya miezi miwili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live