Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Seychelles yatangaza hali ya hatari baada ya kutokea kwa mlipuko mkubwa

Seychelles Yatangaza Hali Ya Hatari Baada Ya Kutokea Kwa Mlipuko Mkubwa Seychelles yatangaza hali ya hatari baada ya kutokea kwa mlipuko mkubwa

Thu, 7 Dec 2023 Chanzo: Bbc

Hali ya hatari imetangazwa nchini Seychelles, baada ya kutokea kwa mlipuko mkubwa katika eneo la viwanda kwenye kisiwa kikuu cha Mahé pamoja na mafuriko.

Rais wa Ushelisheli Wavel Ramkalawan ameamuru raia wote isipokuwa wafanyikazi muhimu kusalia nyumbani.

Watu kadhaa wamejeruhiwa.

Mlipuko huo ulitokea katika kampuni ya ujenzi na uchimbaji mawe, ambapo vilipuzi vilikuwa vikihifadhiwa, na kuacha uharibifu katika eneo la viwanda la Providence.

Uwanja wa ndege wa kimataifa pia uliharibiwa, licha ya kuwa umbali wa kilomita 4 (maili 2.5).

Shule zimefungwa na harakati pekee inayoruhusiwa ni kuingia na kutoka kwa waliokwenye likizo katika visiwa hivyo.

Chanzo: Bbc