Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Seven Mosha boss Sony Music Africa Mashariki

Christine Seven Mosha 1 660x400 Seven Mosha boss Sony Music Africa Mashariki

Wed, 16 Dec 2020 Chanzo: millardayo.com

Sony Music Ent. Afrika imemteua Christine Mosha maarufu Seven kuongoza upande wa Masoko na Maendeleo ya Wasanii kwa Ukanda wa Afrika Mashariki

Mosha ambaye ni Mtanzania atakuwa na jukumu la kuijenga Kampuni hiyo ikiwemo kukuza Wasanii wa Afrika Mashariki na kuwafanya wafanye vizuri ndani na Nje katika level za Kimataifa na atakuwa anaripoti moja kwa moja kwa Sean Watson, Managing Director wa Sony Music Afrika .

“Seven ametumia karibu maisha yake yote kutoa mchango kwenye Muziki wa Afrika , ana passion , na anafaa kuutangaza Muziki wa Afrika Mashariki kwenye Ramani ya Dunia”- Sean Watson

Hivi karibuni Msanii Ommy Dimpoz alitangaza rasmi kuwa ameingia Mkataba na Sony Music Ent. Afrika.BREAKING: MWIGIZAJI JENGUA AFARIKI DUNIA

Chanzo: millardayo.com