Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yaweka ukomo mtu kutoka na fedha nje

E142041a4c2255c9599475d4b73dbf8a Serikali yaweka ukomo mtu kutoka na fedha nje

Tue, 6 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

SERIKALI ya Sudan Kusini imepiga marufuku watu wanaosafi ri nje ya nchi kuondoka na zaidi ya dola za Marekani 10,000, ili kudhibiti kuanguka kwa uchumi.

Waziri wa Habari na Utangazaji, Michael Lueth, ametangaza mkakati huo mpya, akisema umependekezwa na Baraza la Mawaziri baada ya kamati iliyoundwa kuangalia masuala ya uchumi na ukusanyaji mapato yasiyo ya mafuta kutoa ripoti yake.

Alisema kiwango cha juu cha fedha kitakachoruhusiwa kwa wasafiri kwenda nacho nje ya nchi ni dola za Marekani 10,000, baada ya kubainika kuna watu wamekuwa wakisafiri na kiwango kikubwa cha fedha.

“Suala la kuruhusu mtu kuondoka na kiasi kikubwa cha fedha limechangia kumaliza rasilimali na kuidhoofisha Benki ya Sudan Kusini, kwa hivyo suala hilo limekomeshwa kabisa na waziri wa fedha ameamriwa kusitisha utoaji wa wa fedha wa nyongeza,” alisema Makuei.

Waziri huyo alisema serikali pia imekubali kuondoa msamaha wa ushuru kwa bidhaa ambazo sio muhimu zinazoingia nchini kwa nia ya kupanua ukusanyaji wa mapato yasiyokuwa ya mafuta.

“Tumekubaliana kusiwe na msamaha wa ushuru tena ambao unatuondolea mapato,” Alisema.

Aidha, Makuei alisema serikali imepokea dola za Marekani milioni 250 kutoka benki ya African Export and Import (Afreximbank) kwa ajili ya kukabiliana na madhara ya kiuchumi yaliyosababishwa na mlipuko wa ugonjwa wa covid-19.

Alisema malipo ya mkopo huo yatakuwa kwa mfumo wa mafuta na kiasi hicho cha fedha kitatumika kulipia madeni yote ambayo wanatakiwa kulipa ili kuanza upya

Chanzo: habarileo.co.tz