Tue, 1 Aug 2023
Chanzo: Bbc
Serikali imekivunja chama kikuu cha upinzani nchini Senegal kinachojulikana kama PASTEF, baada ya kuzuiliwa kwa kiongozi wake, Ousmane Sonko.
Waziri wa mambo ya ndani alisema chama cha mrengo wa kushoto, cha pan-Africanist kimekuwa kikichochea ghasia wakati wa maandamano ya kuipinga serikali mwezi uliopita.
Bw Sonko amefikishwa mahakamani na kuzuiliwa rumande, akishtakiwa kwa kupanga uasi, njama ya uhalifu na makosa mengine.
Chanzo: Bbc