Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yataifa Sh bil 1 aliyotumiwa na mpenzi wake mzungu

 Felista Nyamathira Njoroge Serikali yataifa Sh bil 1 aliyotumiwa na mpenzi wake mzungu

Fri, 26 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama kuu Nchini Kenya imeiruhusu Serikali ya Nchi hiyo kutaifisha zawadi ya pesa za Kenya milioni 102 milioni (Tsh. Bilioni 1.74) iliyotumwa kutoka Ubelgiji na Bilionea aitwae Marc De Mesel kwenda Kenya kwa Mpenzi wake ambaye ni Felista Nyamathira Njoroge (23) baada ya kubainika kuwa huenda kiasi hicho cha pesa kilitokana na utakatishaji fedha.

Jaji Esther Maina aliamuru kutaifishwa kwa fedha hizo kwasababu chanzo chake kutoka kwa Bilionea Marc hakikuwekwa wazi kama ilivyotakiwa na kusema kutokana na kukosekana kwa taarifa za chanzo cha fedha hizo huenda zimetokana na utakatishaji fedha hivyo akaunti za Benki zichukuliwe kwa Serikali.

Nyamathira ambaye ni Mwanafunzi wa Chuo cha Ufundi Nairobi aligonga vichwa vya habari mwaka 2021 alipofichua kuwa Polisi wameishikilia zawadi ya pesa aliyotumwa na Mpenzi wake aliyepo Ubelgiji.

Vyombo vya Habari Kenya vimeripoti kwamba hii sio mara ya kwanza kwa Tajiri huyo wa Ubelgiji kutuma pesa nyingi Kenya kwani aliwatumia Wanawake wengine watatu jumla ya pesa za kenya milioni 257 ambazo ni zaidi ya Bilioni nne kwa pesa za Tanzania ambapo Mwanamke mmoja Jane Wangui Kago alitumiwa milioni 49 za Kenya, Serah Wambui shilingi milioni 100 na Tabby Wambuku Kago milioni 108.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live