Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yasema marufuku ya miraa na serikali za kaunti sio halali

Serikali Yasema Marufuku Ya Miraa Na Serikali Za Kaunti Sio Halali Serikali yasema marufuku ya miraa na serikali za kaunti sio halali

Tue, 28 May 2024 Chanzo: Bbc

Mafuruku ya matumizi ya muguka, aina ya miraa katika serikali za kaunti sio halali, amesema waziri wa kilimo Mithika Linturi, akieleza kuwa muguka ni zao lililoratibiwa kulingana na Sheria ya Mazao ya 2013 na kanuni za miraa 2023.

Hayo yanajiri baada ya Rais Ruto na uongozi wa Embu kufanya mkutano maalum Jumatatu kujadili kupigwa marufuku kwa muguka katika kaunti kadhaa.

Gavana Cecily Mbarire alikuwa miongoni mwa waliohudhuria mkutano wa Jumatatu katika Ikulu ya Nairobi, pamoja na naibu gavana, seneta, mwakilishi wa wanawake, na wabunge wote wa bunge la kaunti.

Chanzo: Bbc