Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yapiga marufuku safari za ndege kati ya Kenya na Somalia

0fgjhs44bogguc63h Serikali yapiga marufuku safari za ndege kati ya Kenya na Somalia

Tue, 11 May 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Mamlaka ya KCAA Jumanne, Mei 11, ilisitisha safari zote kati ya Kenya na Somalia mara moja

- KCAA ilitangaza kuwa ni ndege tu za medevac na ndege za Umoja wa Mataifa kwenye oparesheni za kushughulikia masuala ya kibinadamu, ndizo zitakazoruhusiwa kuhudumu

- Bado haijulikani kwanini ndege hizo zimesitishwa

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Nchini Kenya (KCAA) Jumanne, Mei 11, ilisitisha safari zote kati ya Kenya na Somalia mara moja.

Taarifa ya KCAA ilitangaza kuwa ni ndege tu za medevac na ndege za Umoja wa Mataifa kwenye oparesheni za kushughulikia masuala ya kibinadamu, ndizo zitakazoruhusiwa kuhudumu.

Bado haijulikani kwanini ndege hizo zimesitishwa.

Hatua hiyo inajiri wiki moja baada ya Serikali ya Shirikisho la Somalia kusema imerejesha uhusiano wake wa kidiplomasia na Kenya.

Mnamo Mei 6, Wizara ya Mawasiliano na Habari ya taifa la Somalia ilisema uhusiano wa kidiplomasia umerejeshwa baada ya Qatar kuingilia kati.

"Serikali ya Shirikisho la Somalia, inatangaza kwamba kwa kuzingatia masilahi ya ujirani mwema, imeanza tena uhusiano wa kidiplomasia na Jamhuri ya Kenya," taarifa kutoka kwa wizara hiyo ilisema.

Mnamo Desemba 2020, Waziri wa Habari wa Somalia Osman Abukar Dubbe alitoa makataa ya siku saba kwa wanadiplomasia wa Kenya wanaoishi Mogadishu kuondoka nchini humo.

Wakati uo huo, Dubbe aliwataka wanadiplomasia wanaoishi Kenya, Nairobi kuondoka na kurejea nyumbani.

Somalia iliongeza kuwa ilizingatia sana kanuni za kudumisha uhusiano wa kirafiki na nchi jirani lakini inaamini kuwa hatua za serikali ya Kenya haziendani na uhusiano wa kidiplomasia unaotambulika kimataifa.

Kwa upande wake, Wizara ya Mambo ya Kigeni ilionyesha kwamba iliipokea taarifa ya Somalia kuanzisha tena uhusiano wao wa kidiplomasia na Kenya.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke